Aliyekuwa mbabe wa kivita Mashariki mwa DRC Thomas Lubanga aachiliwa huru
Imechapishwa:
Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Thomas Lubanga ambaye alikuwa mtu wa kwanza kukamatwa na kufungwa jela na Mahakama ya Kimataifa ya ICC, ameachiliwa huru na Mahakama ya Makla jijini Kinshasa baada ya kumaliza kifungo chake cha miaka 14.
Lubanga alipatikana makosa ya ukukwaji wa haki za binadamu kama mauaji na ubakaji wa raia na kuwatumia watoto wakati akiongoza kundi la waasi la UPC kati ya mwaka 1997 hadi 2007 katika jimbo la Ituri.
Mwezi Julai 2010, majaji waliisimamisha kesi ya Thomas Lubanga kuhusu makosa ya uhalifu wa kivita na kuamuru aachiliwe huru baada ya waendesha mashtaka kukataa kuwasilisha taarifa kwa upande wa utetezi.
Bw Lubanga alikana mara kadhaa kutumia watoto kama wanajeshi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuanzia mwaka 2002 hadi 2003.
Thomas Lubanga aliekuwa kiongozi wa wanamgambo wa Union of Congolese Patriots-UPC aliongoza wanamgambo wa kabila la Hema kupigana dhidi ya watu wa kabila la Lendu.
Ghasia za kugombea ardhi ziligeuka na kuwa vita vya kikabila ambapo takriban watu 50,000 waliuawa na maelfu walibaki bila makazi.