COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Cote d'Ivoire: Rasimu ya marekebisho ya katiba yapitishwa bungeni, upinzani walalama

Rais Ouattara akiongozana na Spika wa Baraza la bunge Aprili 1, 2019.
Rais Ouattara akiongozana na Spika wa Baraza la bunge Aprili 1, 2019. Sia KAMBOU / AFP

Bunge nchini Cote d’Ivoire limepitisha sheria ya kuifanyia marekebisho katiba katika nchi hiyo licha ya kupingwa na wapinzani, ambao walijiondoa katika shuguhuli za bunge wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Rasimu ya marekebisho ya katiba kama ilivyopendekezwa na rais wa Cote d’Ivoire Alassane Drahman Ouattara ilipitishwa Jumanne jana, wakati wa kikao cha wabunge huko Yamoussoukro, licha ya wabunge wa upinzani kutoshiriki vikao vya juma lililopita.

Akizungumzia mpango wa kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo mbele wanadiplomasia wa kigeni katika siku za hivi karibuni, rais Ouattara, alisema marekebisho yaliyopendekezwa yanalenga kuifanya katiba "iwe sawa", bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Kipengele kinachopingwa na wapinzani ni kuteuliwa kwa naibu rais ambaye sasa atakuwa akiteuliwa na rais aliyeshinda uchaguzi pamoja na baraza la seneti, huku wakidai kuwa rais Ouattara analenga kumteua mrithi wake atakayechukuwa madaraka baada ya kukamilisha muhula wake wa pili mwaka 2022.

Ni rasmi sasa Takriban watu milioni 6.3 wamepewa haki ya kupigia kura ya maoni rasimu ya katiba hiyo.

Jumla ya vituo 20,000 vya kupiga kura vitafunguliwa kote nchini kuanzia saa 8.00 asubuhi hadi saa 18.00 jioni.

Matokeo ya kura ya maoni yanatarajiwa kutangazwa rasmi siku ya Jumatatu au Jumanne.