GUINEA-SIASA-USALAMA

Mvutano waibuka kuhusu uchaguzi wa Jumapili Guinea

Raia wa na hofu ya uchaguzi wa JUmapili Machi 22, Guinea.
Raia wa na hofu ya uchaguzi wa JUmapili Machi 22, Guinea. REUTERS/Stringer

Zimesalia saa 48 tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge na kura ya maoni ya Katiba, chaguzi mbili ambazo zimeendelea kuzua mvutano nchini Guinea.

Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa wa upinzani wanaona kwamba hizo ni mbinu za rais Alpha Condé ambaye anataka kuchukulia fursa hiyo kwa kuwania muhula wa tatu kinyume cha sheria mama ya sasa.

Kwa upande wa serikali, wamesema hakuna swali la kuahirishwa kwa matukio hayo muhimu kwa nchi na maandalizi yanaendelea vizuri licha ya janga la Covid-19 ambalo Guinea imethibitisha kesi mbili za maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.

Uchaguzi wa wabunge na kura ya maoni ya Kayiba vimepangwa kufanyika Jumapili Machi 22.

Hata hivyo kiongozi mkuu wa upinzani, Cellou Dalein Diallo, amesema kuwa uamuzi wa serikali wa kuandaa uchaguzi huo hauendani "na hali ya sasa ya kiafya.

"Ni kutowajibika, ni kosa la jinai. Serikali haiwajibikaji, haina hata wasiwasi na maisha na afya ya raia wa Guinea. Alpha Condé anataka tu kuwania muhula wa tatu. Sisi, tunawaambia watu: msendi kupiga kura kwa kuhatarisha afya yenu, ili msihusiki katika jaribio hilo la mapinduzi ya katiba ambayo Alpha Condé anataka kufanya. "

Kwa sasa, janga hilo bado linadhibitiwa, amesema Waziri wa Habari Amara Somparé.