ALGERIA-SIASA-HAKI

Algeria: Viongozi wa zamani katika enzi ya Bouteflika wapewa adhabu kubwa

Mawaziri wakuu wawili wa zamani nchini Algeria wamehukumiwa Jumatano wiki hii na Mahakama ya Rufaa ya Algiers kifungo cha miaka 15 na 12 jela kwa makosa ya ufisadi.

Ahmed Ouyahia na Abdelmalek Sellal, Mawaziri wakuu wa zamani wa Algeria.
Ahmed Ouyahia na Abdelmalek Sellal, Mawaziri wakuu wa zamani wa Algeria. FETHI BELAID, RYAD KRAMDI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Watuhumiwa hao wanashtumiwa kuhusika katika kashfa ya magari na ufadhili haramu wa kampeni ya mwisho ya aliye kuwa rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika, kama walivyofanya viongozi wengine wakubwa 20. Lakini adhabu za baadhi yao zimepunguzwa.

Abelmalek Sellal na Ahmed Ouyahia, mawaziri wakuu wawili wa rais Bouteflika, wamejikuta hukumu yao ya miaka 15 na 12 jela imethibitishwa na Mahakama ya Rufaa. Lakini washtakiwa wengine wenye ushawishi mkubwa wakati huo wamejikuta adhabu zao zikipunguzwa.

Hukumu ya kifungo cha miaka 10 katika mahakama ya mwanzo iliyotolewa dhidi ya mawaziri wawili wa zamani wa viwand imepunguzwa kwa nusu. Hukumu ya Ali Haddad, rais wa zamani wa shirika kubwa la waajiri nchini Algeria, imepunguzwa kutoka miaka saba jela hadi miaka minne.

Kwa jumla, ni karibu viongozi wa zamani wa kisiasa, matajiri wakubwa wenye ushawishi na maafisa wakuu kuhukumiwa na Mahakama ya Rufaa tangu mwanzoni mwa mwezi huu. Wanatuhumiwa kufadhili kampeni ya uchaguzi kwa muhula wa tano wa Abdelaziz Bouteflika mwaka 2019, na ubadhirifu katika sekta ya viwanda na magari .Wote sasa wana siku nane za kukata rufaa kwenye Mahakama ya Juu zaidi nchini Algeria.