Raia waendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi Mali
Tume ya uchaguzi nchini Mali imesema kuwa zoezi la kuhesabu kura linendelea nchini humo ikiwa ni siku moja tu baada ya wananchi kushiriki uchaguzi wa wabunge Jumapili Machi 29, 2020.
Imechapishwa:
Uchaguzi huo, ambao kabla ulipangwa kufanyika mwaka 2018 uliahirishwa mara mbili kwa sababu ya kuongezeka machafuko kwenye majimbo ya kati na Kaskazini ya Mali ambako serikali inapambana na makundi ya itakadi kali.
Ni Uchaguzi unafanyika licha ya taifa hilo la Afrika Magharibi kukabiliwa na changamoto ya usalama, kiongozi wa upinzani kutekwa na maambukizi ya Corona.
Wadadisi wa siasa nchini humo wanasema Uchaguzi huu ni muhimu kwa sababu utasaidia kukabiliana na machafuko na kuleta suluhu ya kisiasa katika maeneo yaliyoathiriwa.
Uchaguzi wa wabunge umefanyika nchini Mali wakati huu serikali ikipambana na virusi vya Corona.
Hadi Jana siku ya Jumapili, taifa la Mali liliorodhesha visa 20 vya wagonjwa wa COVID-19.