DRC-CORONA-AFYA

DRC yakabiliwa na changamoto ya matibabu kwa wagonjwa wa Covid-19

Hatua ya kutotoka nje yaendelea kutekelezwa katika Wilaya ya Gombe huko Kinshasa, Aprili 6, 2020.
Hatua ya kutotoka nje yaendelea kutekelezwa katika Wilaya ya Gombe huko Kinshasa, Aprili 6, 2020. Bienvenu-Marie Bakumanya / AFP

Wakati visa vya maambukizi ya Corona nchini DRC vikifikia zaidia ya 250 kunaripotiwa changamoto ya upatikanaji wa matibabu yanayoweza kuwasaidia wagonjwa wanaonesha dalili za ugonjwa huo.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimetaka mikakati zilizowekwa kupambana na ugonjwa wa Corona kuheshimiwa, zikionya  kwamba mji mkuu wa Kinshasa unatarajiwa kupitia wakati mgumu wa maambukizi zaidi kufikia mwezi ujao.

DRC ina visa 254 vya maambukizi ,Kinshasa ikichangia 21 ya idadi hiyo.

Hivi karibuni mdogo wa babake Rais Tshisekedi, na ambaye pia alikuwa kiongozi wa makazi ya kiraia ya rais huyo, Gérard Mulumba Kalemba alifariki kwa Corona.

Askofu Gérard Mulumba alikuwa na umri wa miaka 83 na alikuwa ni mdogo wa babake Rais Félix Tshisekedi.