Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA-SIASA

Libya yaendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu

Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj  amnyooshea kidole cha lawama Marshal Khalifa Haftar.
Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj amnyooshea kidole cha lawama Marshal Khalifa Haftar. AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Kiongozi wa serikali ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa Fayez al-Sarraj ameapa kuitorejea katika meza ya mazungumzo na kiongozi wa vikosi vya upinzani Khalifa Haftar kwa kuendeleza mashambulizi licha ya taifa hilo kuendelea kukabiliana na janga la Corona.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo Serikali ya Libya inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa imewaachilia huru wamgambo wa kinajihadi waliokuwa wanazuiliwa katika miji miwili ya magharibi nchini humo.

Kuachiliwa huru kwa wapiganaji hao kutoka makundi ya kijihadi waliokuwa wakisaidia serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya, kumezua wasiwasi miongoni mwa wakazi wa miji miwili ya Sorman na Sabratah.

Jumapili, Aprili 13, majeshi ya serikali ya umoja wa kitaifa yalikamilisha operesheni ya kuyadhibiti maeneo ya pwani yote ya magharibi hadi kwenye mpaka wa Tunisia. Maeneo ambayo hapo awali yalikuwa chini ya udhibiti wa vikosi vya Khalifa Haftar.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.