AFRIKA KUSINI-CORONA-AFYA

Afrika Kusini yachukuwa mikakati mipya kupambana dhidi ya Corona katika magereza

Cape Town, Afrika Kusini, Machi 28: Hema zimejengwa ili kuwapokea kwa dharura watu wasio na makazi ili kujaribu kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa covid-19 nchini.
Cape Town, Afrika Kusini, Machi 28: Hema zimejengwa ili kuwapokea kwa dharura watu wasio na makazi ili kujaribu kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa covid-19 nchini. Reuters/ Mike Hutchings

Mamlaka nchini Afrika Kusini zimeanza kuelekeza  mapambano dhidi ya Corona kwenye magereza baada ya wafungwa 59 na wafanyakazi wa gereza 29 kuthibitishwa kuambukizwa katika kipindi cha majuma mawili.

Matangazo ya kibiashara

Serikali imeendelea kupuliza dawa kwenye magereza huku wale walioathirika wakitengwa na kupewa matibabu.

Maafisa wa Afya wamekuwa wakifanya mazoezi ya maelezo ya kukabiliana na virusi vya Corona kwa wiki kadhaa huku wengine wakihudumu masaa mengi katika mikutano ya mtandaoni wakijiandaa na kuimarisha mipango yao ya dharura.

Takriban wiki tano zimepita tangu kisa cha kwanza cha Covid 19 kuripotiwa nchini Afrika Kusini , na kufikia tarehe 28 Mwezi Machi idadi ya maambukizi ilikuwa ikiongezeka.

Lakini tangu wakati huo kila kitu kimekuwa kikiwa sawa na mataifa mengine ambapo visa vimekuwa vikigundulika tarehe sawa.

Lakini Jumamosi iliopita idadi ya visa vya maambukizi ilishuka ghafla kutoka watu 243 kwa siku hadi 17, na hivyo basi kuwa na wastani wa visa 50 vipya kila siku.

Hivi karibuni Rais Ramaphosa alipendekeza kwamba wiki mbili za kujitenga ndio zilizosababisha hali hiyo na aliongeza masharti hayo kutekelezwa kote nchini kwa kuwa yalitarajiwa kukamilika katika kipindi cha wiki moja, hadi mwisho wa mwezi huu.