AFRIKA-WHO-IMF-CORONA-AFYA

WHO: Afrika huenda ikaathirika zaidi na virusi vya Corona

Wadadisi wanasema janga la Covid-19 linatarajiwa kusababisha uchumi wa bara la Afrika kushuka kwa asilimia 1.25 mwaka huu wa 2020.
Wadadisi wanasema janga la Covid-19 linatarajiwa kusababisha uchumi wa bara la Afrika kushuka kwa asilimia 1.25 mwaka huu wa 2020. Getty Images

Shirika la Afya Duniani, WHO, limeonya kwamba bara la Afrika huenda likawa na idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona. WHO inabashiri kuwa hali ikiendelea ilivyo sasa, huenda idadi ya vifo ikafikia laki tatu na watu wengine zaidi ya Milioni 30 kuwa masikini.

Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa Afrika ina vifo karibu elfu moja vinavyohusishwa na Corona, huku watu zaidi ya elfu 19 wakiambukizwa ugonjwa huo.

Wakati huo huo Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, limetaka Afrika isaidiwe kukabiliana na ugonjwa hatari wa Covid-19.

IMF imetoa wito wa msaada wa haraka wa kimataifa kwa nchi za Afrika ambazo zinakabiliwa na janga hilo.

Mkurugenzi mkuu wa IMF Kristalina Georgieva amewaambia mawaziri, maafisa wa Umoja wa Mataifa na wengine kwamba bara la Afrika halina raslimali za kutosha na miundo mbinu ya kutosha ya afya ili kukabiliana na janga hilo na kwamba linahitaji karibu dola bilioni 114.

Maambukizi ya virusi vya Corona kote ulimwenguni sasa yamepindukia milioni 2.18 na watu 150,000 wamepoteza maisha.

Wadadaisi wanasema janga la Covid-19 linatarajiwa kusababisha uchumi wa bara la Afrika kushuka kwa asilimia 1.25 mwaka huu wa 2020.