ALGERIA-CORONA-AFYA-RAMADHANI

Coronavirus/Ramadhani: Algeria yaanza kulegeza vizuizi vya kupambana na Corona

Algeria imelegeza baadhi ya hatua za kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa Waislamu.
Algeria imelegeza baadhi ya hatua za kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa Waislamu. REUTERS

Algeria imepunguza hatua ilizochukuwa katika kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona wakati mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani unaanza leo Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya Waziri mkuu wa Algeria imetangaza kwamba amri ya kutotoka nje usiku itatapunguzwa na kuondoa marufuku ya kutembea iliyowekwa katika mji mkuu wa Algeria, Algiers.

Katika taarifa, mamlaka nchini Algeria imesema marufuku ya kutembea katika Mkoa wa Blida, Kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, itarejelewa na amri ya kutotoka nje kuanzia saa 2:00 mchana hadi 7:00 asubuhi.

Na amri ya kutotoka nje kuanzia saa 3:00 alaasiri hadi saa 7:00 asubuhi, ambayo ilikuwa inatumika katika mikoa tisa ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na mji mkuu Algiers, italegezwa, na kuanzia saa 5 jioni hadi 7 asubuhi.

"Serikali imetoa wito kwa raia kuendelea kuwa makini," imesema taarifa hiyo, huku ikiongeza "Kurekebisha au kuendelea na hatua za karantini itategemea na jinsi hali ya ugonjwa wa Covid-19 itakuwa ikiendelea".

Visa 3,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona vinaripotiwa nchini Algeria, huku watu 407 ndio wameripotiwa kuuawa na ugonjwa huo.