DRC-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa 394 vya maambukizi vyathibitisha DRC

Janga la Corona nchini DRC: Raia wanatakiwa kuwa na kibali rasmi kwa kuweza kutembea katika maeneo yaliyo chini ya vizuizi vya kukabiliana na Covid-19, Gombe, Kinshasa, Aprili 6, 2020.
Janga la Corona nchini DRC: Raia wanatakiwa kuwa na kibali rasmi kwa kuweza kutembea katika maeneo yaliyo chini ya vizuizi vya kukabiliana na Covid-19, Gombe, Kinshasa, Aprili 6, 2020. REUTERS/Kenny Katombe

Watu 48 wamepona tangu kuzuka kwa janga la Covid-19 Machi 10, 2020, huku idadi ya wagonjwa wa Covid-19 ikifikia 394 hadi Aprili 23, kwa majibu wa mamlaka nchini DRC.

Matangazo ya kibiashara

"Kwa jumla, vifo 25 vimeripotiwa na watu 48 wamepona ugonjwa wa Covid-19; watu 212 wanaoshukiwa kuambukizwa virusi vya Corona wanafanyiwa vipimo na visa vipya17 vimethibitishwa jijini Kinshasa; na mtu mwengine ameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupona ugonjwa huo”, ripoti ya sekretarieti ya ufundi imebaini.

Habari njema ni kwamba hakuna vifo vipya kati ya visa hivyo vilivyothibitishwa.

Hata hivyo wagonjwa 246 wa Covid-19 wanaendelea vizuri, kwa mujibu wa Radio ya Umoja aw Mataifa, Okapi, ikinukuu vyanzo rasmi.