DRC-USALAMA-HAKI

Ne Mwanda Nsemi akamatwa DRC

Moja ya makaazi ya kiongozi wa kundi la Bundu dia Kongo, Ne Muanda Nsemi, katika kata ya Joli Parc, wilayani Ngaliema, Kinshasa. makazi yake hayo yalizingirwa na polisi Februari 14, 2017.
Moja ya makaazi ya kiongozi wa kundi la Bundu dia Kongo, Ne Muanda Nsemi, katika kata ya Joli Parc, wilayani Ngaliema, Kinshasa. makazi yake hayo yalizingirwa na polisi Februari 14, 2017. RFI/Sonia Rolley

Polisi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imemkamata Ijumaa hii Aprili 24, 2020 kongozi wa kundi la Bundu dia Kongo Zacharie Badiengela anayejulikana kwa jina la Ne Muanda Nsemi, baada ya operesheni iliyoendeshwa dhidi yake na wafuasi wake.

Matangazo ya kibiashara

Tangu Alhamisi, Aprili 23, 20, polisi walikuwa wamezingira nyumba yake inayopatikana katika eneo la Macampagne katika Wilaya ya Ngaliema.

Hakuna mtu aliyeruhusiwa kutoka au kuingia katika eneo la Macampagne kuelekea kaburi la Kintambo,

Kumekueko na vizuizi kadhaa vilivyowekwa katika mtaa wa Mbenseke ili kuzuia mru yeyote kuingia katika eneo la Macampagne.

Baada ya kushindikana kwa mazungumzo yaliyo dumu masaa kadhaa, polisi imeamua kuendesha operesheni dhidi yake na wafuasi wake leo Ijumaa asubuhi.

Muda mfupi kabla ya kukamatwa kwake, sehemu kubwa ya wafuasi wake ambao wanajulikana kwa jina la "Makiese", ambao walikuwa wanamlindia usalama, wamekuwa tayari wamejisalimisha mikononi mwa polisi wakihofia usalama wao, baada ya kuona idadi kubwa ya maafisa wa polisi waliotumwa katika eneo hilo, kwa mujibu wa Radio ya Umoja wa Mataifa, Okapi.

Kanali Muanamputu, msemaji wa polisi ya DRC, amesema kuwa Ne Mwanda Nsemi amepelekwa mahakamani mara moja.

Hivi karibuni watu zaidi ya14 waliuawa katika mapigano kati ya vikosi vya usalama na watu wanaoshukiwa kutoka kundi la Bundu dia Kongo, linaloongowza na Ne Mwanda Nsemi. Tukio hilo lilitokea kando ya barabara inayounganisha Kinshasa na mji wa Matadi.

Wafuasi wa kundi hilo la kisiasa na kidini wanashtumiwa kuendesha vitendo vya kikatili dhidi ya raia wasio wazaliwa wa eneo hilo.