DRC-KAMERHE-HAKI-UCHUMI

Wanasheria wa Vital Kamerhe wafutilia mbali tuhumu dhidi ya mteja wao

Vital Kamerhe alisimamia mpango wa dharura kwa siku 100 za kwanza katika serikali ya rais Tshisekedi.
Vital Kamerhe alisimamia mpango wa dharura kwa siku 100 za kwanza katika serikali ya rais Tshisekedi. REUTERS/Baz Ratner

Wakati Kesi inayomkabili mkurugenzi wa afisi ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasio ya Congo, Vital Kamerhe ikisubiriwa kusikilizwa ifikapo Mei 11 kufuatia tuhuma dhidi yake kuhusu matumizi mabaya ya pesa za serikali wanasheria wake wana imani kwamba mteja wao aataachiliwa huru.

Matangazo ya kibiashara

Mawakili wake wamesema hakuna ushahidi wowote kuhusu kushirikishwa kwa shemeji yake Soraya Mpiana, katika manunuzi ya uwanja unaomilikiwa na msimamizi mkuu wa kampuni Samibo-Congo, Samih Jammal jijini Kinshasa.

Kwa mujibu wa barua ya mahakama, mbali na mkurugenzi huyo wa afisi ya rais Vital Kamerhe, kesi hii itawashirikisha washtakiwa wengine wawili, Samih Jammal, msimamizi mkuu wa kampuni Samibo Congo Sarl na Husmal Sarl, kampuni ya mafundi wa ujenzi kutoka Uturuki Karmod inayojihusisha na ujenzi wa makazi.

Inadaiwa kwamba Kamerhe pamoja na Samih Jammal, walikubaliana kujenga zaidi ya makazi ya jamii elfu 4,500 katika majimbo matano, na pia kuboresha hali ya makazi ya polisi na wanajeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa.

Samih Jammal, mkuu wa afisi ya rais wa DRC, Pamoja na mshtakiwa wa tatu Jeannot Muhima wanatuhumiwa kutumia zaidi ya dola milioni 50 kati ya milioni 60 zilizotengwa kati ya mwezi Machi na Agosti 2019 katika mpango wa siku 100 wa rais Felix Tshisekedi.

Kesi hii itasikilizwa siku ya Jumatatu Mei 11, katika ukumbi wa Mahakama, wakati huu mawakili wake Vital Kamerhe wakiendelea kukanusha tuhuma dhidi ya mteja wao.