AFRIKA-CORONA-AFYA

Baadhi ya nchi za Afrika zaanza kulegeza masharti ya kusalia nyumbani

Serikali ya Rwanda ilitangaza kwamba kuanzia Jumatatu 04/05/2020, baadhi ya watu wataruhusiwa kuendeleza shughuli zao za kawaida, huku baadhi zikiendelea kufungwa.
Serikali ya Rwanda ilitangaza kwamba kuanzia Jumatatu 04/05/2020, baadhi ya watu wataruhusiwa kuendeleza shughuli zao za kawaida, huku baadhi zikiendelea kufungwa. Simon Wohlfahrt / AFP

Baada ya Ghana, Afrika Kusini na Kenya, hatimaye Rwanda na Nigeria zimeanza kulegeza masharti ya raia kutotembea kama sehemu ya mapambano dhidi ya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Hali ya kawaida imeanza tangu Jumatatu wiki hii nchini Rwanda na Nigeria. Hata hivyo vizuizi hivyo vitakuwa vikiondolewa hatua kwa hatua kadri hali ya Corona itakuwa ikiendelea nchini, mamlaka nchini Rwanda imesema.

Baada ya siku 45 za kusalia ndani, raia wa Rwanda walirejelelea shughuli zao kwa masharti ya kuvaa barakoa na kutokaribiana.

Serikali ya Rwanda ilitangaza kwamba kuanzia Jumatatu 04/05/2020, baadhi ya watu wataruhusiwa kuendeleza shughuli zao za kawaida, huku baadhi zikiendelea kufungwa.

Mikusanyiko bado imepigwa marufuku na kila biashara inayofanywa inatakiwa kutozidisha nusu ya wanaofanya biashara hiyo. Sheria ya kutotoka nyumbani imelegezwa kutokana na kile kinachoonekana kuwa shinikizo za kiuchumi baada ya kutekelezwa kwa zaidi ya wiki sita.

Hata hivyo serikali ilitangaza watu wataruhusiwa kufanya kazi zao lakini hawataruhusiwa kuondoka majumbani kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi na moja asubuhi.

Nchi nyingi barani Afrika zimechukua hatua ya kuweka marufuku ya raia kusalia nyumbani toka mlipuko wa virusi hivyo kuingia barani humo na kuonesha hatari ya maambukizi zaidi ya ndani ya jamii.

Japo hatari ya virusi ingalipo, nchi za Afrika zinalegeza masharti na kuonekana kukabiliana vyema na virusi.