MISRI-CORONA-UCHUMI

Coronavirus: Misri yahofia uchumi wake

Misri, yenye wakazi milioni 100, visa 7,201 vya maambukizi vimeripotiwa nchini humo na watu 452 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa aw Covid-19.
Misri, yenye wakazi milioni 100, visa 7,201 vya maambukizi vimeripotiwa nchini humo na watu 452 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa aw Covid-19. © AFP

Baada ya kulegeza hatua zake dhidi ya ugonjwa hatari wa Covid-19, Misri inatarajia kurudi kwa hali ya kawaida ili kuondokana na madhara ya janga la ugonjwa huo kwenye uchumi wake, baada ya kukabiliwa kwa miaka kadhaa na mgogoro wa kisiasa.

Matangazo ya kibiashara

Kutokana na mgogoro wa kiafya duniani, Cairo imeamua kudumisha shughuli katika sekta kadhaa ili kuweka sawa ukuaji wa mazao yake ya ndani (GDP), ambayo yalifikia 5.6% mwishoni mwa mwaka wa 2019 kulingana na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Kama sekta ya ujenzi, kilimo na uchumi zinaendelea kufanya kazi bila vizuizi vingi, sehemu kubwa ya viwanda, utalii na mamlaka ya anga vimekwama.

Sekta ya utalii, ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Msri, tayari imekumbwa na mgongano wa kisiasa na usalama baada ya maamndamano ya raia ya mwaka 2011.

Mnamo mwaka wa 2019, sekta hii muhimu iliingiza euro bilioni 11.6 katika mapato, ikiwa ni faida kubwa zaidi kwa muongo mmoja, kulingana na takwimu za serikali.

Uchumi wa Misri ulipanda zaidi baada ya mageuzi yaliyowekwa mnamo mwaka 2016 kama sehemu ya mpango wa msaada wa IMF wa dola bilioni 12 ( sawa na euro bilioni 10.7).

Mnamo mwezi Januari, Misri ilikuwa kati ya nchi kumi zilizoinuka kiuchumi duniani, kulingana na utafiti uliofanywa na Benki ya Standard Chartered huko London.

Lakini baada ya kuzuka kwa ugonjwa wa Covid-19, Cairo ilitangaza hatua ya watu kubaki nyumbani, viwanja vya ndege kufungwa, migahawa, shule na vyuo vikuu kufungwa, mamilioni ya watumishi wa umma wakaachishwa kazi na biashara zote kufungwa.

Misri, yenye wakazi milioni 100, visa 7,201vya maambukizi vimeripotiwa nchini humo na watu 452 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa aw Covid-19.