COTE D'IVOIRE-SORO-SIASA-HAKI

Cote d'Ivoire: Chama cha Guillaume Soro chakabiliwa na mashitaka

Richard Adou, Mwendesha mashitaka katika mahakama ya Abidjan, le Machi 22 2016.
Richard Adou, Mwendesha mashitaka katika mahakama ya Abidjan, le Machi 22 2016. SIA KAMBOU / AFP

Wiki moja baada ya Guillaume Soro kuhukumiwa na mahakama ya jinai ya Abidjan kifungo cha miaka ishirini, mwendesha mashtaka Richard Adou amekishtumu chama cha waziri mkuu wa zamani Guillaume Soro kutaka kuhatarisha usalama wa taifa.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka Richard Adou, uchunguzi katika kipindi cha miezi michache iliyopita uliwezesha kupatikana katika eneo la Assinie bunduki 50 aina ya Kalashnikov, buduki kubwa za kivita 12, bunduki kubwa 4, pamoja na risasi na vifaa kadhaa vya jeshi vilivyofichwa hapo na waasi.

Pia kulingana na Richard Adou, silaha hizi zililetwa hapo kwa magari 4 ya mtu aitwaye Zébré Souleymane, ambaye kwa sasa yuko mafichoni.

Mwendesha mashitaka amebaini kwamba awali silaha hizo zilihifadhiwa kwenye makao makuu ya chama cha GSP cha Guillaume Soro.

"Uchunguzi ulibaini kuwa makao makuu ya chama hiki cha siasa yalitumika kuhifadhi silaha," amesema mwendesha mashtaka Richard Adou. Viligunduliwa pia kwenye makao makuu ya chama hicho vifaa vingi vya mawasiliano ya kijeshi na nyaraka ambazo yanaonyesha vitendo na malengo ya ya chama hicho cha kisiasa."

Tayari watu 19 ikiwa ni pamoja na askari 14, wakiwemo maafisa wa juu 2 wamekamatwa.

Baadhi ya askari waliokuwa katika kikosi cha ulinzi cha Guillaume Soro ni miongoni mwa waliokamatwa.