Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA-RUSHWA-HAKI

Kesi ya Jacob Zuma yasogezwa mbele hadi Juni 23

Jacob Zuma, mbele ya tume ya kupambana na ufisadi huko Johannesburg, Julai 19, 2019.
Jacob Zuma, mbele ya tume ya kupambana na ufisadi huko Johannesburg, Julai 19, 2019. REUTERS/Mike Hutchings

Kesi kuhusu ufisadi inayomkabili rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma, iliokuwa imepangwa kusikilizwa Jumatano wiki hii, imeahirishwa hadi Juni 23 kwa sababu ya janga la Corona, upande wa mashtaka umetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Zuma, mwenye umri wa miaka 78, anashutumiwa kuwa alipokea rushwa kutoka kwa kampuni ya elektroniki na ulinzi Thales katika mkataba wa silaha wenye thamani ya Rand milioni 4, karibu euro 216,000 kwa bei ya sasa, uliyotolewa mwaka 1999.

Jacob Zuma na kampuni ya Thales wameendelea kukanusha tuhuma hizo.

Mpango wa silaha ulifanyika mwaka 1999 mwaka ambao bwana Zuma alihama kutoka mkuu wa jimbo kuwa makamu wa rais.

Anashtakiwa kwa kukubali kuchukua malipo yasiyokuwa halali 783

Mshauri wake wa mambo ya fedha ,Schabir Shaikh alikutwa na hatia kwa kujaribu kuomba rushwa kwa niaba ya bwana Zuma kutoka katika kampuni ya silaha za Ufaransa na kosa hilo lilipelekea akafungwa jela mwaka 2005.

Kesi dhidi ya bwana Zuma ilifutwa muda mfupi kabla hajawania nafasi ya uraisi mwaka 2009.

Tangu kushtakiwa kwa mara kwanza, Jacob Zuma alitumia njia zote za kisheria zinazowezekana kujaribu kufutilia mbali kesi hiyo, bila mafanikio.

Hata hivyo, wiki iliyopita, Jacob Zuma alitangaza kwamba atakata rufaa kwa Korti ya Katiba, mahakama ya juu zaidi nchini, na hivyo kufunguwa njia ya kesi yake kusikilizwa upya mbele ya mahakama ya Pietermaritzburg (kaskazini mashariki) Mei 6.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.