DRC-UCHUMI-HAKI

Kesi ya "mpango wa siku 100" DRC: Waziri wa Elimu ya Ufundi kushtakiwa

Mahakama Kuu huko Kinshasa nchini DRC
Mahakama Kuu huko Kinshasa nchini DRC RFI/Habibou Bangré

John Ntumba, Waziri wa sasa wa Elimu ya Ufundi na mshirika wa karibu wa mkurugenzi kwenye afisi ya rais, Vital Kamerhe, anafanyiwa uchunguzi katika kesi ya mpango wa siku 100 wa rais Felix Tshisekedi.

Matangazo ya kibiashara

John Ntumba ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya ufuatiliaji ya mpango wa dharura wa Félix Tshisekedi anashtumiwa, kama kiongozi wake katika chama cha UNC, makosa ya ubadhirifu wa mali ya umma.

Mwanasheri Mkuu wa Serikali katika Mahakama ya Juu amemtaarifu Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga Ilunkamba hali hiyo kwa barua.

John Ntumba anatuhumiwa ubadhirifu katika mpango huo wa rais, kabla ya kuteuliwa kushika nyadhifa serikalini mwezi Agosti mwaka uliopita. Wakati huo alikuwa na majukumu ya kufuatilia utekelezaji wa kazi ya "siku mia moja" katika Mkoa wa Kasai ya Kati, ngome yake wakati wa uchaguzi.

Katika mkoa huo, pia moja ya ngome za rais Félix Tshisekedi, kulikuwa kumepangwa hasa kufanyiwa ukarabati wa barabara, madaraja lakini pia ujenzi wa visima vya maji, shule, makazi ya jamii na hata bwawa la umeme. Lakini tangu wakati huo, hakuna kilichojengwa.

Gavana wa mkoa huu, Martin Kabuya, amekuwa akiumwa kwa miezi. Kwa kizuizi hiki cha Waziri John Ntumba, mwisho wake ulikuwa na mshikamano juu ya usimamizi wa fedha zilizopewa Kasaï-Central."

Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Mahakama ya Juu tayari ameanzisha uchunguzi na anasubiri idhni kutoka kwa Bunge la Kitaifa kumuitisha John Ntumba ili aweze kusikilizwa kwa mara ya kwanza. Licha ya kuwa mahakama haijatangaza kiasi cha fedha zilizopitishwa mlango wa nyuma, Gavana wa Mkoa wa Kasai ya Kati Martin Kabuya amebaini kwamba dola milioni 32 zilizotolewa na serikali tangu mwaka jana kwa shughuli za kukarabati miundombinu katika mkoa huo "zilimezwa" na "hakuna kilichofanyika".

John Ntumba alikataa kuzungumza na RFI alipotafutwa. Lakini wiki mbili zilizopita, alitangaza kutokuwa na hatia na kuahidi kushirikiana na mahakama.