NIGERIA--CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Raia 265 wa Nigeria warejeshwa nyumbani

Nigeria inaendelea kushuhudia ongezeko la maambukizi ya Corona ambayo yamefikia karibu Elfu tatu na vifo vipya vya watu 98.
Nigeria inaendelea kushuhudia ongezeko la maambukizi ya Corona ambayo yamefikia karibu Elfu tatu na vifo vipya vya watu 98. Reuters

Nigeria imeanza kuwarudisha nyumbani raia wake waliokwama katika mataifa ya kigeni kutokana na janga na Corona, na kushindwa kusafiri kutokana na vikwazo vya kufanya hivyo.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la kwanza ni Wanaigeria 265 ambao walirejea siku ya Jumatano wiki hii wakitokea Dubai na kufikia katika mji wa Lagos, huku kundi la pili la watu 300 likitarajiwa kurejea nytumbani siku ya Ijumaa wakitokea jijini London nchini Uingereza.

Wizara ya Mambo ya Nje katika taarifa yake imesema kuwa raia wengine wa Nigeria wanatarajiwa kurudi nyumbani siku ya Jumapili wakitokea jijini New York nchini Marekani.

Baada ya kuwasili nyumbani, raia hao watalazimika kukaa karantini kwa siku 14 kabla ya kuruhusiwa kwenda kuonana na wapendwa wao.

Wanarejea nyumbani, wakati huu nchi yao ikiendelea kushuhudia ongezeko la maambukizi ya Corona ambayo yamefikia karibu Elfu tatu na vifo vipya vya watu 98.