UN-DUNIA-NJAA-CORONA-USALAMA

Coronavirus: Umoja wa Mataifa wahitaji Dola Bilioni 4.7 kusaidi nchi masikini

Wanawake na watoto ndio wa kwanza kuathiriwa na njaa.
Wanawake na watoto ndio wa kwanza kuathiriwa na njaa. (cc)unocha

Umoja wa Mataifa unaomba msaada wa Dola Bilioni 4.7 kuyasaidia mataifa masikini katika kipindi hiki ambacho dunia inapambana na janga hatari la Covid-19.

Matangazo ya kibiashara

Huu ni wito  mwingine wa Umoja wa Mataifa, ambao hapo awali ulikuwa umeomba msaada mwingine wa Dola Bilioni 2 mwezi Machi.

Mkuu wza Tume inayoshughulikia misada ya kibiandamu OCHA Mark Lowcock amesema fedha hizo zitakwenda kwa mataifa masikini yanayohitaji msaada wa haraka.

Lowcock amesema kuwa iwapo hatua za haraka hazitachykuliwa, huenda kiwango cha njaa na umasikini kikaongezeka maradufu katika mataifa hayo.

Mataifa zaidi ya 20 hasa barani Afrika yanaelezwa na OCHA yakiwepo yale yanayoshuhudia ukosefu wa usalama kama Syria na Afganistan.

Umoja wa Matafa unawatalea wito wahisani kujitokeza kwa haraka ili kuyaepusha mamilioni ya watu kukabiiana na baa la njaa.