CHAD-CORONA-AFYA

Coronavirus: Wakazi wa Ndjamena na miji mikubwa ya Chad marufuku kutembea

Chad inataka kuzuia kuenea kwa virusi kwa kupiga marufuku wakazi wa miji yake kutembea, ikiwa ni pamoja na mji mkuu Ndjamena (picha ya kumbukumbu).
Chad inataka kuzuia kuenea kwa virusi kwa kupiga marufuku wakazi wa miji yake kutembea, ikiwa ni pamoja na mji mkuu Ndjamena (picha ya kumbukumbu). Xaume Olleros/Bloomberg via Getty

Serikali ya Chad imechukua hatua ya kudhibiti maambukizi ya Corona katika mji mkuu wa nchi hiyo Ndjamena na miji mingine mikubwa. Marufuku ya watu kutotembea katika miji hiyo inaanza kutumika leo Ijumaa Mei 8.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inalenga kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona katika miji mingine wakati nchi hii imethibitisha visa 256 vya maambukizi na vifo 27. Kwa upande wa baadhi ya wataalamu, uamuzi huu unakuja umechelewa.

Kuanzia Ijumaa hii na kwa wiki mbili mfululizo, wakazi wa mji mkuu wa Chad, Ndajamena na miji mingine mikubwa wametakiwa kubaki ndani. Magari yanayosafirisha bidhaa yameruhusiwa kuingia tu katikati ya miji kuanzia saa 4:00 usiku, sawa na saa mbili baada ya kumalizika kwa muda wa kutotoka nje, ambao unaanza saa 2:00 usiku hadi saa 11:00 asubuhi.

Hii ni kuzuia virusi kusambaa amesema Waziri wa Afya, Profesa Mahmoud Youssouf Khayal.

"Amri hii ya 38 ambayo tumetia saini inahusu miji yote mikuu ya mikoa na jiji la Ndjamena, nina maanisha miji yetu yote. Hii ni kuzuia virusi kusambaa. (…) Hizi ni hatua za kuzuia virusi kusambaa bain ya binadamu", ameongeza waziri Mahmoud Youssouf Khayal.

Chad imethibitisha visa vipya 83 vya maambukizi, idadi ambayo inafanya visa vya maambukizi kufikia jumla ya 253, huku idadi ya vifo ikifikia 30. Kiwango cha vifo ambacho kimeelezewa, kulingana na wataalamu, na ukosefu wa vipimo vya jumla na kutofuata hatua za kudhibiti ugonjwa huo.