MSUMBIJI-VYOMBO VYA HABARI-HAKI-USALAMA

Hofu yatanda baada ya kutoweka kwa mwandishi wa habari Msumbiji

Des soldats mozambicains en patrouille à Mocimboa da Praia, dans le nord du pays, le 7 mars 2018
Des soldats mozambicains en patrouille à Mocimboa da Praia, dans le nord du pays, le 7 mars 2018 © AFP

Ni mwezi mmoja sasa tangu mwandishi wa habari Ibraimo Mbaruco kutoweka Kaskazini mwa Msumbiji, eneo linaloendelea kukumbwa na machafuko baada ya kuzuka uasi wa wanamgambo wa Kiislamu.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Msumbiji linanyooshewa kidole kuhusika na tkio hilo.

Kwa miaka kadhaa, Ibraimo Mbaruco amekuwa mwandishi wa habari wa radio moja ya serikali akitoa taarifa za mji wa Palma, karibu na mpaka wa Tanzania.

Katika miaka michache, kijiji hiki cha uvuvi chenye utulivu katika mkoa wa Cabo Delgado kiligeuka kuwa makao makuu ya makampuni kutoka Marekani au Ufaransa ambayo yalitarajia kutumia hifadhi kubwa ya gesi ya chini ya maji iliyoko katika pwani za kiji hicho.

Kwa miaka miwili na nusu, mkoa huo pia umekuwa ukikaliwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu ambalo linadai kuwa na mafungamano na kundi la Islamic State, kwa lengo la kudhibiti eneo hilo lenye Waislamu wengi na kulifanya kuwa makao yake makuu mapya.

Mbali na machafuko hayo, Ibraimo Mbaruco mara ya mwisho mashahidi wanasema walimuona Aprili 7 karibu saa 12:00 jioni alipokuwa akitoka kazini akirudi nyumbani huko Palma.

Dakika chache baadaye, aliwmtumia ujumbe mmoja kati wenzake akimweleza kwamba "amezingirwa na askari". Tangu wakati huo, hajarudi kuonekana na simu yake imezimwa.

Wanahabari wenzake na mashirika yasiyo ya kiserikali wananyooshea kidole cha lawama vikosi vya usalama kuhusika na tukio hilo.