Pata taarifa kuu
LIBYA-USLAMA

Libya: Mji mkuu wa Libya wakumbwa na mashambulizi mabaya ya angani

Tripoli baada ya mashambulizi yaliyotekelezwa na vikosi vya Marshal Khalifa Haftar, Mei 9, 2020.
Tripoli baada ya mashambulizi yaliyotekelezwa na vikosi vya Marshal Khalifa Haftar, Mei 9, 2020. Mahmud TURKIA / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Zaidi ya makombora mia moja yalirushwa katika mji mkuu wa Libya, Tripoli, na kusababisha vifo vya watu wanne na kuharibu vibaya uwanja wa ndege.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yalitekelezwa mwishoni mwa wiki na majeshi ya NLA ya Khalifa Haftar ambayo yanajaribu kudhibiti mji wa Tripoli tangu Aprili 4, 2019.

Mwishoni mwa wiki hii wakazi wa mji wa Tripoli hawakutoka ndani kutokana na makombora ambayo yalikuwa yakirindima katika mji huo.

Vikosi vya Khalifa Haftar vilirusha makombora kadhaa katika maeneo yenye makazi ya Abu Salim na Ben Gachir, Kusini mwa mi wa Tripoli. Raia wanne, ikiwa ni pamoja na msichana wa miaka 5, waliuawa.

Uwanja wa ndege wa Mitiga Kaskazini Magharibi pia ulishambuliwa kwa makombora hayo yaliyorushwa Jumamosi na Jumapili. Ndege mbili ziliteketea kwa moto, ukumbi wa abiria kupumzikia pia uliharibiwa vibaya. Ghala nne za mafuta kati ya kumi ziliteketea kwa moto, na sita zingine ziliharibiwa vibaya, kwa mujibu wa kampuni ya taifa ya mafuta.

Uwanja wa ndege umefungwa kwa miezi kadhaa sasa kutokana na mashambulizi ya angani ya mara kwa mara, lakini hii ni mara ya kwanza hasara kama hizo kutokea.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.