LESOTHO-CORONA-AFYA

Coronavirus: Kisa cha kwanza cha maambukizi chathibitishwa Lesotho

Moja ya mitaa mikuu ya mji mkuu wa Lesotho, Maseru.
Moja ya mitaa mikuu ya mji mkuu wa Lesotho, Maseru. Photo: Michael Denne, source: Wikipedia

Lesotho imetangaza kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya Corona. Lesotho ilikuwa nchi pekee ya Afrika ambayo ugonjwa huo ulikuwa bado kuripotiwa.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya ya Lesotho imesema imefanya vipimo 81 kwa madereva kutoka Afrika Kusini na Saudi Arabia, na mmoja wao amekutwa na virusi vya Corona. Matokeo ya vipimo vingine 301 yanatarajiwa kutolewa.

Lesotho nchi inayopakana na Afrika Kusini, ilikuwa nchi pekee ya Afrika ambayo ugonjwa huo ulikuwa bado kuripotiwa. Kufikia sasa watu zaidi ya 10,000 wameambukizwa virusi vya Corona.

Kulingana na ripoti ya shirika la habari la Reuters ikijikita takwimu rasmi na data kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO), Afrika ina watu, 69,764 waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona na watu 2,421 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Mlipuko huo, ulioibuka katikati mwa China, huko Wuhan mwezi Desemba, kufikia sasa umeathiri nchi 210 kote duniani, huku kukiripotiwa visa milioni 4,8 vilivyothibitishwa na vifo 290,868, kulingana na takwimu za shirika la habari la Reuters likijikita data rasmi.