DRC-ITURI-USALAMA

Ituri: Saba wauawa katika mapigano kati ya jeshi na waasi Ituri

Askari wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakiwa vitani huko Matombo, kilomita 35 kaskazini mwa Beni, Kaskazini-Magharibi mwa DRC, Januari 13, 2018.
Askari wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakiwa vitani huko Matombo, kilomita 35 kaskazini mwa Beni, Kaskazini-Magharibi mwa DRC, Januari 13, 2018. AFP

Raia saba wameauwa na wanajeshi zaidi ya 12 kujeruhiwa katika mkoa wa Ituri, Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, katika mashambulizi yaliyotokea Jumanne usiku ambayo pia yamesababisha kuwepo kwa idadi kubwa ya wakimbizi.

Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi waliojeruhiwa, wameondolewa katika eneo hilo na ndege ya kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO.

Kwa mujibu wa Radio ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, Okapi, askari kumi na tatu wa FARDC ndi waliojeruhiwa wakati wa mapigano dhidi ya kundi la wanamgambo wa CODECO katika eneo la Djugu, katika jimbo la Ituri, Kaskazini- Mashariki mwa DRC.

Hata hivyo kulingana na vyanzo vya jeshi, askari hao walijeruhiwa Jumapili Mei 10 wakati wa mapigano yaliyotokea katika msitu mmoja huko Djugu baada ya kuwatimu wanamgambo wa kundi la CODECO kutoka eneo la Bese. Waliondolewa kwenye eneo hilo na wenzao hadi katika kijiji cha Dala na kisha kusafirishwa kwa gari kwenda Mongwalu.

Msemaji wa jeshi huko Ituri, Luteni Jules Ngongo, amekaribisha "msaada wa MONUSCO" kwa FARDC kumaliza mgogoro wa kivita huko Ituri. Luteni Jules Ngongo amebaini kwamba kitendo hicho kizuri cha MONUSCO cha mara kwa mara kinaokoa maisha ya askari wa FARDC ambao walikuwa kwenye dhiki kwenye uwanja wa vita.

Wanajeshi wengine waliojeruhiwa walisafirishwa wiki iliyopita hadi Bunia, kwa kutumia helikopta za MONUSCO, kutoka Roe katika eneo la Djugu.