BURKINA FASO-USALAMA

Jeshi la Burkina Faso lawapoteza askari wake 8 katika shambulizi

Jeshi la Burkina Faso likipiga doria karibu na kambi ya kikosi cha jeshi la ulinzi wa taasisi, RSP, Septemba 29, 2015.
Jeshi la Burkina Faso likipiga doria karibu na kambi ya kikosi cha jeshi la ulinzi wa taasisi, RSP, Septemba 29, 2015. AFP PHOTO / SIA KAMBOU

Maafisa wa jeshi nchini Burkina Faso wamethibitisha kuuawa kwa askari wanane wa nchi hiyo mwanzoni mwa juma hili katika shambulio lililotekelezwa na wapiganaji wa kijihadi eneo la Kaskazini mwa Burkina Faso karibu na mpaka wa Niger.

Matangazo ya kibiashara

Askari wanane wa Burkina Faso waliuawa Jumatatu katika shambulio la kijihadi huko Kankanfogouol, mji wa Kaskazini mwa Burkina Faso, karibu na mpaka wa Niger, vyanzo vya usalama vililiambia shirika la Habari la AFP Jumanne wiki hii.

Mapema vyanzo vya usalama vilisema Jumatatu kuwa askari wasiopungua wanne waliuawa na wanne wamekosekana katika shambulio la kijihadi.

"Miili ya askari waliokosekana ilipatikana wakati wa operesheni ya jeshi ya kuwasaka wanajihadi hao, na kufanya idadi ya askari waliouawa kufikia wanane," kilisema chanzo cha usalama.

Shambulio hilo lilitokea Jumatatu wakati "timu kutoka kwa jeshi la Sebba, lililokuwa likipiga doria, lilijikuta katika hali tete ya kushambuliwa kundi la magaidi wenye silaha huko Kankanfogouol", chanzo cha usalama kililiambia shirika la habari la AFP.

"Kankanfogouol iko kilomita chache kutoka Niger na makundi ya silaha yanapita kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine wa mpaka, kufanya mashambulizi katika nchi zote mbili," chanzo hicho kimeongeza.

"Dharura ya kiafya iliyohusishwa na mapigano yasiyokoma dhidi ya Covid-19 haipaswi kutufanya tusahau umuhimu wa usalama. Tunapaswa kuendelea kuwa macho kwa pande hizi mbili, na ningependa hapa kupongeza vikosi vyetu. Ulinzi na Usalama, "Rais wa Burkina Faso, Roch Marc Christian Kaboré, aliandika kwenye Twitter, lakini hakuelezea shambulio hilo.