COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Mrithi wa Amadou Gon Coulibaly kujulikana hivi karibuni

Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara Machi 16, 2020.
Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara Machi 16, 2020. RFI

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara, ambaye hivi karibuni alitangaza kwamba atafanya mabadiliko madogo katika serikali yake, ana mpango wa kumteua waziri mkuu mpya kuchukua nafasi ya Amadou Gon Coulibaly.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na gazeti la JeuneAfrique, mabadiliko hayo muhimu kwenye uongozi wa serikali yanapaswa kufanywa mara tu atakaporejea Amadou Gon Coulibaly, ambaye anapumzika kwa wiki kadhaa huko Paris, nchini Ufaransa baada ya kusafiri huko kwa matibabu.

Awali Amadou Gon Coulibaly alitamani kushikilia wadhifa wake hadi utakapofanyika uchaguzi wa urais nchini humo, huku akiachia baadhi ya majukumu yake kwa wasaidizi wake wenye ushawishi mkubwa.

Hata hivyo ameunga mkono mpango huo wa Alassane Ouattara (ADO). Kama mgombea na mwenyekiti wa bodi ya uongozi wa Chama cha RHDP, madarakani, hatimaye atajikita kwenye kampeni yake ya uchaguzi.

Rais Ouattara kwa sasa yuko njia panda kwa kumteua waziri mkuu mpya atakayechukuwa nafasi ya Amadou Gon Coulibaly, ambaye kwa sasa nafasi yake inashikiliwa na Waziri wa Ulinzi, Hamed Bakayoko.