Nigeria yawapoteza askari wake 5 katika shambulio
Imechapishwa:
Wanajeshi watano wa Nigeria wameuawa na wanajihadi Kaskazini kwa taifa hilo baada ya kambi yao kushambuliwa. Wanajihadi hao kutoka Kundi la ISWAP wametekeleza shambulizi hilo katika kituo cha ukaguzi wa magari eneo la Mainok katika jimbo la Borno.
Machafuko ya wa hivi karibuni yalisababisha watu wengine wengi kuyatoroka makazi yao na kufanya zaidi ya watu 60,000 kutoroka eneo la Kaskazini-Magharibi mwa Nigeria tangu kutokea kwa mara ya kwanza tukio kama hilo la watu kuyatoroka makazi yao mnamo mwezi wa Aprili 2019.
Watu wanaotafuta ulinzi wanaruhusiwa kuingia nchini Niger licha ya kufungwa mipaka kwa sababu ya janga la Covid-19.
Kulingana na ushuhuda uliokusanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi, ukosefu wa usalama ndio ulisababisha watu 23,000 kutoroka makazi yao kaskazini-Magharibi mwa Nigeria na kukimbilia nchini Niger mwezi uliyopita.