DRC-KAMERHE-UCHUMI-HAKI

Mpango wa siku 100 DRC: Mpwa wa Vital Kamerhe akamatwa

Vital Kamerhe, mkurugenzi kwenye ofisi ya rais wa DR Congo, Félix Tshisekedi.
Vital Kamerhe, mkurugenzi kwenye ofisi ya rais wa DR Congo, Félix Tshisekedi. RFI/Sonia Rolley

Mpwa wa Vital Kamerhe, Daniel Massaro, yuko mikononi mwa vyombo vya dola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu Ijumaa , Mei 15.

Matangazo ya kibiashara

Daniel Shangalume Nkingi anatarajiwa kufikishwa kwenye ofisi ya mashitaka Jumatatu wiki ijayo. Anashukiwa kumkutanisha mkurugenzi wa ofisi ya rais Tshisekedi na mfanyabiashara kutoka Lebanon Samih Jammal katika shughuli kuhusu mkataba wa ujenzi wa nyumba na kunufaika kwa matumizi mabaya ya fedha za umma katika sehemu ya mpango wa siku 100 wa rais Felix Tshisekedi. Kesi ambayo inawakabili mjomba wake Vital Kamerhe na Samih Jammal.

Daniel Shangalume Nkingi, alias Massaro, amepatikana nje kidogo ya mji mkuu Kinsaha karibu na eneo la Bateke.

Shangalume Nkingi ambaye anahusika na masuala ya tathmini katika Wizara ya Bajeti, alipotea siku ambayo alikuwa anatarajiwa kusikilizwa kw Kinshasa-Matete, Aprili 9, siku moja baada ya kukamatwa kwa mjomba wake.

Vital Kamerhe anatuhumiwa kupitisha mlango wa nyuma zaidi ya dola milioni 50 kwa jumla ya dola Milioni 500 zilizotengwa kwa mpango wa rais wa "siku 100" .

Kesi ya Vital Kamerhe iliahirishwa hadi Mei 25 mwaka huu.