DRC-ITURI-USALAMA

DRC: Ishirini waangamia katika shambulizi jipya Ituri

Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006.
Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006. REUTERS

Mashambulizi ya watu wenye silaha yanaendelea kusababisha vifo kuhujumu usalama wa raia katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Ituri, Kaskazini-Mashariki mwa DRC.

Matangazo ya kibiashara

Watu wasiopungu 20 waliuawa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili katika shambulio jipya katika eneo la Djisa huko Djugu. Wanamgambo wa kundi la Codeco wanashtumiwa kuhusika na shambulio hilo.

Washambuliaji kadhaa walishambulia eneo hilo hilo na kuua watu karibu ishirini kwa mapanga.

Watoto, wanawake na wazee ni miongoni mwa watu waliouawa katika shambulio hilo. Watu kuumi na saba waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali ya Drodro, eneo linalopatikana kilomita 70 kutoka Bunia, mji mkuu wa mkoa wa Ituri. Jeshi linaendelea kuwasaka wanamgambo wa kundi hilo.

Hili ni sambulio la pili ndani ya wiki moja. Shambulio hili jipya limezua sintofahamu katika eneo la Djisi, huku mashirika ya kiraia katika eneo hilo yakishtumu vikosi vya jeshi katika vijiji jirani vya Masumboko na Largo kwamba havikuingilia kati mapema kunusuru maisha ya watu waliouawa.

Jeshi linasema halikuweza kuingilia kati mapema kwa sababu washambuliaji hawakutumia silaha za moto.