Vikosi vya usalama na ulinzi vya Burkina Faso vyashtumiwa kuwaua watu 12 wasiokuwa na hataia
Imechapishwa:
Wiki iliyopita watu 12 wanaoshtumiwa kuwa magaidi walifariki katika mazingira tatanishi wakiwa kizuizini katika makao makuu ya polisi ya Tanwalbougou kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa Faso katika Mahakam ya Fada.
Kulingana na wanaharakati wa haki za binadamu, mazingira ya vifo vya watu 12, usiku wa Mei 11 kuamkia Mei 12, yanatakiwa kuwekwa wazi.
Wanaharakati hao wa Haki za binadamu wamebaini kwamba bila shaka watu hao 12 waliuawa tu kwa kisingizio cha vita dhidi ya ugaidi.
Baada ya uchunguzi zaidi, mbunge Aziz Diallo aligundua mwili wa binamu yake katika chumba cha kuhifadhi maiti cha mji wa Fada.
"Aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani. Sikufungua mifuko mingine ili niseme kwamba wote waliuawa kwa kupigwa risasi kama ndugu yangu. Lakini kile tulichokiona, hata kwenye makaburi, ni kwamba wote walikuwa na majeraha kichwani. Ni jambo lisiloeleweka, kuchukuwa watu kuwauwa kwa risasi bila kuwafikisha mahakamani, kwa kisingizo kuwa ni katika vita dhidi ya ugaidi, " amesema mbunge Aziz Diallo.
Kwa upande wa wakili Ambroise Farama kutoka mashirika ya haki za binadamu nchini Burkina Faso, anasema kukosekana kwa uchunguzi na utambulisho wa miili hiyo kunatoa shaka juu ya utashi wa mamlaka ya mahakama kutoa mwanga juu ya kesi hiyo.
"Waliwekwa kizuizini polisi kwa gerearmerie brigade, ambayo inamaanisha kuwa hawakuweza kujitetea, kwa hivyo hakuna chochote cha kuelezea kwa nini walipatikana wakiwa wamekufa siku iliyofuata. Lakini mwendesha mashtaka anasema wangekufa kutokana na kutosheleza. Katika kesi hiyo, mwendesha mashtaka, ikiwa kweli alikuwa anataka kufanya uchunguzi mzito, angekuwa tayari alidai kutokuwa na sheria, "alisema Maître Ambroise Farama.JaridaPokea habari zote za kimataifa moja kwa moja kwenye sanduku lako la baruaNinajiungaKwa upande wa serikali, hakuna majibu ya mashtaka yake. Wanasema wanangojea hitimisho la uchunguzi uliofunguliwa na mwendesha mashtaka wa Faso.
"Walifariki dunia usiku kwa kukosa hewa walipokuwa wakizuiliwa sehemu moja," kilisema chanzo cha usalama, kabla ya taarifa kutoka kwa mwendesha mashitaka. Chanzo hicho kimeongeza kuwa waliokamatwa walipaswa kuhojiwa kabla ya kupelekwa katika jela kuu.
Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, watu ishirini na tano walikamatwa na vikosi vya ulinzi na usalama usiku wa Mei 11 kuamkia Mei 12. Watu hao ambao walikuwa wakishtumiwa ugaidi, walikuwa kizuizini katika kituo cha polisi huko Tanwalbougou, kilomita 40 kutoka mji wa Fada N'Gourma.