Pata taarifa kuu
DRC-UCHUMI

DRC yafuta uamuzi wa kusitisha ushuru wa mapato

Eneo la kibiashara ya Kinshasa huko DRC, katika Wilaya ya Gombe.
Eneo la kibiashara ya Kinshasa huko DRC, katika Wilaya ya Gombe. REUTERS/Kenny Katombe
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeamua kufuta uamuzi wa awali uliositisha zoezi la ukusanyaji wa mapato (IPR) wakati nchi hiyo inaendelea kukumbwa na janga la Covid-19.

Matangazo ya kibiashara

Tangu mwezi Aprili mwaka jana, mamlaka, ambayo ilitaka kupunguza athari zinazotokana na janga la Covid-19 kwa wafanyakazi wa umma, iliamua kufuta ushuru wa 15% ya mshahara na marupuru ya watumishi wa umma na maafisa wa serikali.

Hatua hiyo ilichukuliwa mwishoni mwa mwezi Machi na serikali ya DRC. Hatua ya kusitishwa kwa ushuru wa mapato ilitarajiwa kutumika kwa kipindi cha miezi mitatu, kuanzia malipo ya mshahara wa mwezi wa Aprili. Ushuru wa mapato utaanza kukusanywa tena kuanzia malipo ya mwisho wa mwezi wa Mei.

Mamlaka ya mapato imebaini kwamba hatua hiyo ya serikali inakuja kumaliza hali tete iliyoshuhudiwa katika mamlaka hiyo tangu serikali kuchukuwa hatua yake ya kufuta ushuru wa mapato kutokana na janga la Covid-19.

Kulingana na mmoja wa wakurugenzi wa mamlaka hiyo ya kifedha, hatua hiyo ilisababisha upungufu mkubwa katika hazina ya serikali, sawa na zaidi ya dola milioni 11.

Katika barua yake ya kutangaza kuanza tena zoezi la kukusanya ushuru, Waziri wa Fedha, José Sele Yalaghuli ameelezea uhusiano kati ya serikali na Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF. Kinshasa iliahidi IMF kwamba itaongeza mapato, ikiwa ni pamoja na kupanua wigo katika masuala la ushuru, IPR.

Taasisi hii yafedha ya kimataifa pia iliomba serikali ya DRC, kabla ya kukubaliwa kuwa kwenye mpango wake mpya, kwanza kusimamia vizuri matumizi yake na kuwa wazi zaidi. DRC kwa sasa inakabiliwa na ukosefu wa mapato, baada ya mipaka yake kufungwa pamoja na uzalishaji mdogo wa madini.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.