Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA-USALAMA

Uteuzi wa mwenyekiti mpya wa Tume ya Uchaguzi wazua sintofahamu Guinea

Makao makuu ya CENI huko Conakry, Guinea.
Makao makuu ya CENI huko Conakry, Guinea. DR
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Uteuzi wa jaji Mamadi 3 Kaba kama Mwenyekiti mpya wa Tume Huru ya Uchaguzi, CENI, umeibuwa mjadala mkubwa nchini Guinea. Upinzani wa kisiasa unapinga kuteuliwa kwake, ukimchukulia kuwa ni mtu wa karibu na serikali.

Matangazo ya kibiashara

Mamadi 3 Kaba aliteuliwa Alhamisi Mei 14 na sheria ya rais, akichukua nafasi ya Wakili Salif Kébé, aliyekuwa mwenyekiti wa tume hiyo na ambaye alifariki dunia Aprili 17 kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Mabishano makubwa yameibuka kwenye chama cha Mawakili nchini Guinea, ambacho kinashikilia uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Katiba Mei 4. Kufuatia kifo cha Wakili Salif Kébé, Mahakama ya Katiba iliona kuwa nafasi yake kama mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi inapaswa kujazwa na mtu mwengine ambaye atateuliwa na chama cha Mawakili kama ilivyokuwa kwa uteuzi wa Wakili Salif Kébé.

Lakini baada ya kuona kuwa sheria ya kirais ndio imemteua Mamadi 3 Kaba kujaza nafasi ya Wakili Salif Kébé, chama cha Mawakili kimebaini kwamba "hakikutendewa haki". "Siasa zimengia kazi ya mahakama, viongozi wanataka Tume Huru ya Uchaguzi iwe chini ya himaya yao," mmoja wa mawakili amesema.

Hata upinzani umekosoa utaratibu huo wa uteuzi wa mwenyekiti mpya wa CENI, huku ukiomba mtu asiegemea upande wowote kutoka mashirika ya kiraia, ndiye ateuliwe kwenye nafasi hiyo.

Upinzani unasema Mamadi 3 Kaba ni "mwanaharakati anayejulikana kuwa ni mfuasi wa chama cha RPG.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.