AFRIKA KUSINI-CORONA-AFYA

Afrika Kusini hatarini kwa vifo vingi na maambukizi zaidi katika siku za usoni

Wanasayansi nchini Afrika Kusini wanaonya kuwa huenda watu 50,000 wakapoteza maisha na wengine zaidi ya Milioni tatu, kuambukizwa virusi vya corona kufikia mwisho wa mwaka huu.

Afisaa wa afya wakati wa kampeni ya kupima virusi vya Corona huko Lenasia, Afrika Kusini Aprili 21, 2020.
Afisaa wa afya wakati wa kampeni ya kupima virusi vya Corona huko Lenasia, Afrika Kusini Aprili 21, 2020. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Onyo hili limekuja wakati huu Afrika Kusini ikiendelea kuongoza kwa visa vya maambukizi vya Corona barani Afrika, ikiwa na maambukizi 18,000 huku watu 339 wakipoteza maisha.

Wizara ya afya nchini humo iliwaajiri Wanasayansi hao kutoa taswira ya maambukizi hayo, na kubainika kuwa huenda kati ya watu 35,000 na 50,000 wakapoteza maisha kufikia mwezi Novemba.

Raia wa Afrika Kusini, kwa wiki ya nane sasa, wameendelea kusalia nyumbani katika vita dhidi ya mamabukizi hayo, hatua ambayo serikali nchini humo inasema imesaidia kupunguza maambukizi hayo.