TANZANIA-KENYA

Tanzania, Kenya zatafuta suluhu ya madereva mpakani wakati huu wa Corona

Wataalamu wa afya kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania wa LungaLunga wakipuliza dawa katika malori. 19/05/2020
Wataalamu wa afya kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania wa LungaLunga wakipuliza dawa katika malori. 19/05/2020 Joseph Jira/RFI

Madereva wa malori ya kubeba mizogo eneo la Afrika Mashariki wanalalamikia zoezi la kupima virusi vya corona maeneo ya mipakani wakidai linachukua mda mrefu kutoa matokeo ya vipimo.

Matangazo ya kibiashara

Katika mpaka Kenya na Tanzania eneo la Lunga Lunga kuna msongamano mkubwa wa malori, madereva hapa wakiarifu kuwa wamesubiri kwa muda mrefu kapata matokeo ya vipimo vya ugonjwa wa corona ili kuendelea na safari.

"Mimi naitwa kamau joseph nilipima hapa tarehe 13 nikaambiwa results zinatoka baada ya masaa 48 sasa kila siku naenda pale na bado mpaka wa leo hazijapatikana".

"Natoka Tanzania naelekea lunga lunga perani, leo nasiku ya 4 nasubiri majibu hapa, sasa hatujui kinachoendelea ni kitu gani mpaka saa hizi, twasubiri nmatokeo ya Kenya kama turudi Tanzania kama tuendelee na safari".

Suleiman Chehe ni afisa wa forodha mpakani lunga lunga akishulika na maswala ya afya.

"Wakenya kama wameeka mikakati yao inabidi mfuate masharti yao ,mwenye ambae anapenda kupima na anapenda kazi yake nendeni mkapime, mwenye hataki abaki".

Serikali kupitia kamishna wa kaunti ya Kwale kusini mwa pwani Karuku Ngumo anasema wanajitahidi kutatua tatizo hilo mpakani ili kupunguza msongamno wa malori.

"Inabidi tukichukua zile samples tunapeleka mpaka kilifi so inachukua muda kiasi tuko na hospitali kubwa sana hapa msambweni, tutajaribu kuzungumza na governor na waziri wa afya tuone kama tunaweza kufanya hiyo hospitali ikuwe kituo pia cha kufanyia uchunguzi wa  virusi vya corona".

Msongamano huo unatokana na mikakati ya serikali kupunguza kusambaa kwa virusi vya corona.

Habari hii imeandaliwa na mwandishi wetu wa Mombasa, Joseph Jira