DRC-ICC-BEMBA-HAKI

ICC yafutilia mbali ombi la Jean-Pierre Bemba la kufidiwa

Jean-Pierre Bemba (katikati anavaa shati ya rangi ya kijani), Juni 23, 2019 alipofika Kinshasa.
Jean-Pierre Bemba (katikati anavaa shati ya rangi ya kijani), Juni 23, 2019 alipofika Kinshasa. ALEXIS HUGUET / AFP

Jean-Pierre Bemba amekwamishwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), ambapo alidai kulipwa karibu euro milioni 70 kama fidia kwa mali zake zilizoharibiwa kipindi chote alikuwa jela.

Matangazo ya kibiashara

Jean-Pierre Bemba ambaye alishtakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka 2002 na 2003, aliachiliwa huru mwezi Juni 2018.

Jean-Pierre Bemba hajafanyiwa unyonge na mahakama, " majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) wamesema katika uamuzi wao wa Mei 18.

Makamu wa rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) hataweza kupata euro milioni 26.2 alizo dai kulipwa na Mahakama ya ICC kwa miaka yote alipokuwa kizuizini katika jela la Scheveningen.

Jean-Pierre Bemba alikamatwa katika kitongoji cha Brussels mwezi Mei 2008, na kufungwa miaka kumi.

Katika uamuzi uliotolewa Mei 18, majaji walibaini kwamba "miaka 10 ni muda wa kifungo kwa mtu aliyewafanyia mateso watu wengine.

Lakini majaji wamesema Jean-Pierre Bemba amesikilizwa mara kwa mara mahakamani na hawezi kupata fidia.