ALGERIA-USALAMA-SIASA

Wapinzani waendelea kukamatwa Algeria

Maandamano dhidi ya serikali huko Algiers, Februari 28, 2020 (picha ya kumbukumbu).
Maandamano dhidi ya serikali huko Algiers, Februari 28, 2020 (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Ramzi Boudina

Nchini Algeria, wanaharakati wa vuguvugu la Hirak wanaendelea kudai kuachiliwa huru wale wote wanaozuiliwa baada ya kushiriki maandamano.

Matangazo ya kibiashara

Mashirika mengi ya kutetea haki za binadamu yamebaini kwamba ikiwa maandamano ya kila wiki yamesimamishwa tangu Machi 20, kwa sababu ya hali ya kiafya inayotokana na janga la Corona, shinikizo na visa vya kamata kamata vikiendelea.

Tangu mwanzoni mwa wiki hii, angalau watu watatu wamekamatwa na mamlaka ya Algeria kwa sababu ya habari walizochapisha kwenye mitandao ya kijamii. Mahakama ilitoa hukumu dhidi ya watu hao ya kifungo hadi miezi 18, kwa kosa la "taarifa ambazo zinaweza kuhatarisha usalama wa taifa" au "kumkashifu rais wa Jamhuri".

Shirika la kimataifa lma Haki za Binadamu, Amnesty International imebaini kwamba kumeongezeka shinikizo tangu kuzuka kwa mgogoro wa kiafya, kwa kuwakamata watu wanaotumia mtandao wa kijamii wa Facebook, na sio tu wanaochapisha habari.

Picha na jina la Walid Kechida vimeendelea kuzunguka kwenye mitandao ya kijamii, katika wiki za hivi karibuni. Kijana huyu wa miaka 25, mwanaharakati wa vuguvugu la Hirak, anazuiliwa huko Setif tangu Aprili 27, kwa sababu ya kuchapisha habari kama hizo na kuweka picha zinazotusi viongozi. Anatuhumiwa kutusi viongozi na rais wa Jamhuri. Anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitano.