DRC-KAMERHE-UCHUMI-HAKI

Mpango wa siku 100: Kesi ya Vital Kamerhe kuanza tena kusikilizwa

Vital Kamerhe alikuwa akisimamia mpango wa dharura wa siku 100 ambao umemtia matatani na kutuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umaa.
Vital Kamerhe alikuwa akisimamia mpango wa dharura wa siku 100 ambao umemtia matatani na kutuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umaa. REUTERS/Baz Ratner

Kesi ya Vital Kamerhe na washtakiwa wenzake inatarajiwa leo Jumatatu kuanza tena kusikilizwa huko Kinshasa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa ofisi ya rais Felix Tshisekedi anatuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kupitisha mlango wa nyuma milioni 50 Dola za Marekani, zilizotengwa kwa ununuzi na ujenzi wa nyumba za maafisa wa jeshi na polisi nchini DRC.

Baada ya kusikilizwa kwa mara ya kwanza Mei 11, mambo muhimu katika kesi hiyo yanaanza na Jumatatu hii.

Tangu kusikilizwa kwa mara ya mwisho, Daniel Shamgalume anayejulikana kwa jina la "Massaro", mtuhumiwa ambaye alikuwa anakosa katika kesi hiyo, anayeshtumiwa kukutanisha mjomba wake Vital Kamerhe na mfanyabiashara kutoka Lebanon Jammal Sammih, alikamatwa mapema wiki hii.

Hata hivyo Daniel Shamgalume hatasikilizwa moja kwa moja katika kesi ya leo inayomhusu mjomba wake, ingawa labda anaweza kuitwa kama shahidi, kulingana na upande wa utetezi wa Vital Kamerhe.

Wakati huo huo wanasheria wa Jammal Sammih, wanashtumu kwamba walichelewa kupata vitu 2,368 kwenye faili ya mteja wao, lakini wanasema hawawezi kuomba kesi hiyo iahirishwe.

Wanasheria wa serikali wanaonya kwamba orodha ya mashahidi inaweza kuwa refu wakati upande wa utetezi wa Vital Kamerhe ukibaini kwamba mchakato huo "umeharakishwa".

Tayari vitali Kamerhe amekataliwa mara kadhaa kuachiliwa kwa dhamana, sawa na mfanyabiashara kutoka Lebanon ambaye amerejeshwa gerezani tangu mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya wiki kadhaa kufanyiwa matibabu katika mji mkuu wa Kinshasa.