Pata taarifa kuu
SUDAN-BASHIR-UCHUMI-HAKI

Sudan: Karibu dola bilioni 4 zakamatwa kutoka kwa rais wa zamani Al-Bashir na ndugu zake

Rais wa Sudan Omar Al-Bashir akilihutubia taifa katika ikulu ya rais Ijumaa, Februari 22, 2019.
Rais wa Sudan Omar Al-Bashir akilihutubia taifa katika ikulu ya rais Ijumaa, Februari 22, 2019. ASHRAF SHAZLY / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Habari hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki hii na Kamati inayopambana dhidi ya Rushwa iliyoteuliwa mwezi Desemba ili kuangamiza mfumo wa rais Omar Al- Bashir aliyetimuliwa mamlakani.

Matangazo ya kibiashara

Omar Al-Bashir bado anazuiliwa, na kesi zaidi bado zinamsubiri.

Dola bilioni 3.5 hadi 4 zilikamatwa katika kipindi kisichozidi miezi sita kwenye kutoka kwake Bashir na ndugu zake. Mali hizo zilizokamatwa ni pamoja na pesa, mali zisizohamishika na hisa katika makampuni mbalimbali, amesema Salah Manaa, msemaji wa Kamati inayopambana dhidi ya rushwa.

Tangu kukamatwa kwa rais wa zamani miezi 13 iliyopita, operesheni ya kukamata mali za rais huyo imeendelea kukamatwa. Karibu dola milioni 130 zilipatikana zimefichwa kwenye mifuko nyumbani kwake. Tangu wakati huo, mali za chama chake, vyombo vya habari, na marafiki na jamaa zake zimezuiliwa au kukabidhiwa Wizara ya Fedha.

Omar Al Bashir ambaye alihukumiwa miaka miwili mwezi Desemba, bado anazuiliwa katika jela la Kober huko Khartoum. Na taratibu zingine zinatarajiwa, amesema Mohamed al-Faki. Kulingana na mwakilishi huyu wa Kamati, mashtaka mapya yataanza hivi karibuni kuhusu utakatisha wa fedha, rushwa au hata kujitajirisha kinyume cha sheria. Taasisi hiyo pia itaangalia kesi ya maafisa wa zamani waliofukuzwa madarakani na serikali ya zamani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.