Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA-HAKI

CAR: Mahakama Maalum ya jinai yawashikilia wanamgambo wa kundi la UPC

Jaji Mkuu wa Mahakama Maalum ya Jinai (CPS) Michel Landry Louanga, (picha ya kumbukumbu).
Jaji Mkuu wa Mahakama Maalum ya Jinai (CPS) Michel Landry Louanga, (picha ya kumbukumbu). Gaël Grilhot/RFI
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Mahakama Maalum ya jinai, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, imetangaza kuwa inawashikilia wapiganaji 9 kutoka kundi la watu wenye silaha la UPC, wanaohusishwa makosa mbalimbali.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama Maalum ya jinai, mahakama ya mseto iliyozinduliwa rasmi mwezi Oktoba 2018 ili kuhukumu uhalifu mkubwa uliotendeka katika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu mwaka 2003 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Operesheni hiyo ya kamata kamata imefanyika kufuatia shambulio lililotokea katika miji kadhaa Kusini-Mashariki mwa nchi hiyo, hasa katika maeneo ya Obo, Bambouti na Zemio - ambapo shambulio la mwisho lilifanyika Mei 19. Mashambulio ya kundi la UPC yanayolaaniwa na Mahakama Maalum ya Jinai, SPC, kama "yanawalenga raia"

"Kama sehemu ya hatua za dharura za muda, wapiganaji 9 kutoka kundi hili lenye silaha wamekamatwa na kupelekwa makao makuu ya SPC kwa lengo la uchunguzi," amesema mwendesha mashtaka maalum.

Mashambulio ambayo kundi la waasi la UPC limekana kutekeleza katika taarifa ya Mei 20.

Katika taarifa yake, SPC inakumbusha kuwa tayari imewaonya wale wanaohusika katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria za kimataifa za kibinadamu katika maeneo haya. Pia imewataka raia "kujitolea kabisa,kuwa makini na kutoa ushirikiano wao napolisi, jeshi na vyombo vya sheria. "

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.