Pata taarifa kuu
DRC-ITURI-MAUAJI-USALAMA

Sitini wauawa katika kipindi cha wiki moja Mashariki mwa DRC

Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006.
Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006. REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Visa vya mauaji vinaendelea kuripotiwa Mashariki mwa DRC, hasa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri. Kundi la wanamgambo la Codeco linashtumiwa kuhusika na mauaji hayo mkoani Ituri, huku kundi la waasi wa Uganda la ADF likibeba mzigo wa lawama Kivu Kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati watu 14 waliuawa Jumatatu asubuhi wiki hii katika vijiji vya Kechele na Makutano katika Mkoa wa Ituri, Kaskazini Mashariki mwa DRC, duru rasmi zimethibitisha.

Hata hivyo wanaharakati wa haki za binadamu wamebaini kwamba idadi ya watu waliouawa katika shambulio hilo ni 17, na kufanya idadi ya waliouawa kufikia 60 katika kipindi cha wiki moja. Pia waasi 17 waliuawa katika mapigano na jeshi, duru hizo zimeongeza.

Tangu Mei 18 hadi Jumatatu Mei 25 sio chini ya watu 60 ambao wameuawa na zaidi ya 70 kutekwa nyara katika katika vijiji tisa vya mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri. Visa vya uporaji na kuunguza magari vimeripotiwa pia katika mikoa hiyo.

Vijiji vya kutano na Kechele vimerekodi idadi kubwa ya mauaji katika kipindi cha wiki moja, kama alivyobainisha Paul Yofe, kiongozi wa Tarafa ya Walese Vonkutu Mkowani Ituri.

Takriban watu 14 waliuawa na waasi baada ya kuwachinja. Tukio hilo lilitokea saa tatu asubui hadi saa Saba mchana katika maeneo ya Bandavilemba kwa sasa hakuna shughuli yoyote katika eneo hilo kwa sababu raia wamelazimika kuyatoroka makazi yao wakihofia kuuawa, " amesema Paul Yofe.

Wakati huo huo jeshi la FARDC limedai kuendesha vita na waasi hao, ili kuhakikidsha kuwa usalama unarejea katika vijiji hivyo.

Raia wanaendelea kutoroka makazi yao kufuatia kuzorota kwa usalama.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.