Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-MAUAJI-HAKI

Mwendesha mashitaka afutilia mbali madai ya kuuawa kwa risasi wafungwa 12 nchini Burkina Faso

Watu 12 waliokamatwa mashariki mwa Burkina na vikosi vya usalama walifariki wakiwa kizuizini (picha ya kumbukumbu)
Watu 12 waliokamatwa mashariki mwa Burkina na vikosi vya usalama walifariki wakiwa kizuizini (picha ya kumbukumbu) Bill Gentile/Gettyimages
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Kiongozi wa mashtaka nchini Burkinafaso  amesema uchunguzi wa awali wa vifo vya wafungwa 12 waliokufa wakiwa kizuizini haujabainisha chanzo cha vifo hivyo.

Matangazo ya kibiashara

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linasema ni njama ya kuficha ukweli.

Watu hao 12 waliokufa wakiwa kizuizuni ni miongoni mwa watu 25 waliokuwa wamepatikana na makossa ya ugaidi.

Wafungwa 12 waliokuwa wakizuiliwa katika kituo cha polisi cha Tanwalbougou katika mkoa wa mashariki mwa Burkina Faso wamepatikana wamekufa katika jela hilo. Tukio hilo lilitokea usiku wa Mei 11 kuamkia Mei 12 walipokuwa kizuizini.

Awali chanzo cha usalama kilibaini kwamba watu hao walifariki dunia kwa kukosa hewa.

Tayari vikosi vya usalama na ulinzi vya Burkina Faso vimeshtumiwa kuwaua watu hao 12 ambao hawakuwa na hatia yoyote.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.