Pata taarifa kuu
DRC-UN-HAKI-MAUAJI-USALAMA

Umoja wa Mataifa waonya kuhusu uhalifu wa kivita Kaskazini Mashariki mwa DRC

Walinda amani wa Monusco wakipiga doria katika mitaa ya eneo la Djugu, katika mkoa wa Ituri, unaoendelea kukumbwana machafuko ya kikabila, Machi 13, 2020.
Walinda amani wa Monusco wakipiga doria katika mitaa ya eneo la Djugu, katika mkoa wa Ituri, unaoendelea kukumbwana machafuko ya kikabila, Machi 13, 2020. SAMIR TOUNSI / AFP

Umoja wa Mataifa umonya kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa makosa ya uhalifu wa kivita Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya watu kadhaa kuuawa na makundi ya watu wenye silaha.

Matangazo ya kibiashara

Mauaji, vitendo vya kikatili, ubakaji na vitendo vingine vinavyokiuka sheria za haki za binadamu vimekuwa sugu na vinatekelezwa na wanamgambo wenye silaha Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), hasa kabila la Walendu, vinaweza kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, Umoja wa Mataifa ulibaini Jumatano wiki hii.

Katika ripoti yake , Ofisi ya Pamoja ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UNJHRO) imebaini kwamba watu wasiopungua 296 waliuawa, wengine 151 walijeruhiwa na 38 walibakwa, wakiwamo wanawake na watoto. Vitendo hivyo vya kikatili vilitekelezwa na waasi kutoka kabila la Walendu kati ya mwezi Novemba mwaka uliopita na mwezi Aprili mwaka huu, kulingana na ripoti ya UNJHO.

Baada ya miaka kadhaa ya utulivu, ghasia za kikabila zimeongezeka tangu mwezi Desemba 2017, hasa kutokana na mizozo ya ardhi.

Maelfu ya wakimbizi, kama katika kambi hii ya wakimbizi ya huko Bunia, Ituri Juni 21, 2019, wakikimbia mapigano makali yaliyotokea Kaskazini mwa DRC.
Maelfu ya wakimbizi, kama katika kambi hii ya wakimbizi ya huko Bunia, Ituri Juni 21, 2019, wakikimbia mapigano makali yaliyotokea Kaskazini mwa DRC. SAMIR TOUNSI / AFP
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.