Pata taarifa kuu
DRC-CORONA-AFYA

Coronavirus: Serikali ya DRC yatangaza masharti mapya wakati wa mazishi

Ugonjwa wa Covid-19 waendelea kuiathiri DRC katika sekta mbalimbali.
Ugonjwa wa Covid-19 waendelea kuiathiri DRC katika sekta mbalimbali. Bienvenu-Marie Bakumanya / AFP

Tangu kuripotiwa kwa visa vya maambukizi ya corona nchini DRC, masharti mapya yametangazwa na serikali hasa kipindi cha mazishi ili kuepusha maambukizi zaidi.

Matangazo ya kibiashara

Watu wasiozidi Ishirini ndio wanaoruhusiwa kuhudhuria mazishi. Atakayekiuka hatua hiyo watashukuliwa hatua za kisheria, serikali ya DRC imetangaza.

Wakati huo huo maafisa wa afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanasema watu 400 waliokuwa wameambukizwa virusi vya Corona wamepona.

Kwa mujibu wa maafisa hao, watu zaidi ya Elfu Mbili na mia nane wameambukizwa virusi vya ugonjwa wa Covid-19, ambao umesababisha vifo vya watu 69 .

Katika hatua nyingine, baadhi ya raia hawakupokea vizuri hatua ya serikali ambayo imetangaza utaratibu mpya wa mazishi hasa jijini Kinshasa huku waombolezaji wasiozidi 20 wakiruhusiwa kushiriki lengo likiwa ni kuepusha maambukizi zaidi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.