COTE D'IVOIRE-ICC-GBAGBO-HAKI

ICC yalegeza masharti ya Gbagbo na Blé Goudé, sasa wako huru kutembea

Charles Blé Goudé (kushoto) na Laurent Gbagbo (kulia), Hague (picha ya kumbukumbu).
Charles Blé Goudé (kushoto) na Laurent Gbagbo (kulia), Hague (picha ya kumbukumbu). Peter Dejong / POOL / AFP/ Montage RFI

Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC, imesema rais wa zamani wa Cote d'Ivoire  Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé wanaweza kuondoka nchini Ubelgiji na Hague chini ya masharti.

Matangazo ya kibiashara

Mwaka uliopita, Laurent Gbagbo na waziri wake wa vijana Charles Blé Goudé walifutiwa mashitaka kufuatia kuhusu vifo vya zaidi ya watu 3,000 wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi nchini mwake 2010.

Msemaji wa Mahakama hiyo amesema Gbagbo mwenye umri wa miaka 73 yuko huru na anaweza kwenda katika taifa analotaka iwapo taifa hilo litamruhusu.

Laurent Gbagbo ambaye kwa sasa yuko nchini Ubelgiji na Charles Blé Goudé ambaye yuko Hague wanaweza kwenda katika nchi 134 ambazo zilitia saini kwenye mkataba wa Rome unaunda Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, bila hofu yoyote ya kukamatwa.

Uamuzi huo wa ICC umepokelewa kwa vifijo na nderemo na wafuasi wa chama cha FPI cha Laurent Gbagbo nchini Cote d'Ivoire.