MADAGASCAR-CORONA-AFYA

Rais Rajoelina abadili msimamo kuhusu mpango wa kuanzisha sindano za dawa ya mitishamba

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina azindua dawa ya mitishamba, akidai kwamba inatibu ugonjwa wa Covid-19, 20 Aprili 2020.
Rais wa Madagascar Andry Rajoelina azindua dawa ya mitishamba, akidai kwamba inatibu ugonjwa wa Covid-19, 20 Aprili 2020. © AFP / Rijasolo

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina anaonekana kubadili imani kuhusu upatikanaji wa dawa ya mitishamba inayoaminiwa kutibu virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka kitengo cha utafiti wa kimatibabu nchini humo kwa niaba ya rais, imesema hapakuwa mipango ya kuanza kutumika dawa ya Artemesia kwa njia ya sindano.

Taasisi ya kitaifa ya matibabu nchini Madagascar pia ilitilia shaka uwezo wa dawa hiyo iliotengenezwa kutoka kwa mmea wa pakanga, ikisema huenda ikaathiri afya ya binadamu.

Hatua hiyo inawadia wakati ambapo marais karibu wanne wa Afrika walidaiwa kuagiza kiasi kikubwa cha dawa hiyo wakiamini kwamba inatibu ugonjwa aw Covid-19.

Awali rais wa Madagascar Andry Rajoelina alikuwa akiisifu na kuikuza dawa hiyo kwani pia aliwakosoa wakosoaji wa dawa hiyo ya mitishamba akisema ni tabia ya ubwenyenye wa mataifa ya magharbi dhidi ya Afrika.

Msimamo huo wa rais wa Madagascar uliungwa mkono na baadhi ya marais wa Afrika wakisema kuwa wao tayari kuiagiza dawa hiyo na wagonjwa kuanza kuitumia katika nchi zao.

Hivi karibuni Shirika la Afya Duniani WHO, lilionya kutoweka imani zao kwa dawa za mitishamba zinazotengenezwa na wenyeji kwa misingi ya kudai kukabiliana na virusi vya Corona.