Pata taarifa kuu
BURUNDI-KENYA

Mke wa rais wa Burundi aendelea kupatiwa matibabu ya Corona, Kenya

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza na mkewe, Denise Nkurunziza, wakiwa mjini Bujumbura 13/10/2017
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza na mkewe, Denise Nkurunziza, wakiwa mjini Bujumbura 13/10/2017 STR / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Baada ya vyombo mbalimbali vya habari kuthibitisha kuza mke za rais za Burundim Pierre Nkurunziza, Denisem yuko kza matibabu nchini Kenyam vyanzo ndani ya Serikali ya Burundim vimekanusha kuwa anasumbuliwa na maradhi ya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa ambazo zilianza kuenea kama uvumi, hatimaye ni wazi sasa mke za rais za Burundi, yuko nchini Kenya, akiendelea kupatiwa matibabu ambayo Serikali ya Burundi inasema sio Corona, huku vyanzo nchinik Kenya vikithibitisha kuwa ni ugonjwa wa Covid 19.

Shirika la habari la Ufaransa, AFP, lilimnukuu afisa mmoja kwenye uwanja wa Melchior nchini Burundi, akithibitisha kuwa Denise alisafirishwa kwenda nchini Kenya na ndege ya shirika la kiafya AMREF.

Vyanzo katika wizara ya afya nchini Kenya, ambavyo havikutaka majina yao kutajwam vimethibitiha kuwa mke wa rais Nkurunziza, yuko nchini humo akisumbuliwa na maradhi ya kupumua ambayo yanahusishwa moja kwa moja na ugonjwa wa Corona

Kuumwa kwa mke wa rais kunathibitidha hatari ya virusi hivyo nchini Burundi, taifa ambali ni miongoni mwa nchi ambazo hazijatangaza makataa ya watu kukusanyika wala kutembea kujaribu kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo.

Juma moja lililopita nchi hiyo ilifanya uchaguzi wake mkuu huku mikutano ya kisiasa ikishuhudia mamia ya watu wakijitokeza bila kuzingatia maelekezo ya shirika la afya duniani kuhusu kujikinga.

Awali rais Nkurunzizam alidai kuwa nchi yake haina haja ya kuweka makataa zozote kwa kuwa inalindwa na Mungum akitupilia mbali madai ya hatari ya virusi vya Corona.

Mwezi uliopitam Serikali ya Burundi ilitangaza kuwafukuza nchini mwake wataalamu 6 wa shirika la afya kwa kile kinachodaiwa kuwa utawala wa Bujumbura haukupenda tathmini zilizofanywa na wataalamu hao kuhusu nchi hiyo kujiandaa kukabili janga la Corona.a

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.