Thelathini na tano wauawa katika mashambulizi Burkina Faso
Imechapishwa:
Hali ya usalama inaendelea kudoroa katika baadhi ya maeneo nchini Burkina Faso. Mashambulizi nchini humo yamesababisha watu wengi kupoteza maisha na wengi kuyatoroka makazi yao, na kukimbilia maeneo salama.
Karibu watu 35 waliuawa katika mashambulizi yaliyotekelezwa katika vijiji viwili nchini Burkina FasoShambulio moja liliendeshwa Mashariki na lingine Kaskazini mwa nchi, serikali imebaini.
"Tulizika miili 37 jioni ya Jumamosi wakati magaidi hao walipoondoka," amesema mkazi mmoja. Kulingana na vyanzo kadhaa, zoezi la kuwatafu baadi ya watu ambao bado wanakosekana linaendelea.
Machafuko haya yanaonyesha jinsi gani hali ya usalama inatisha katika baadhi ya maeneo ya nchi. Makundi ya wanamgambo wa Kiislamu yananyooshewa kidole kuhusika na mashambulizi hayo.
Katika taarifa yake, serikali ilibaini kwamba watu 25 waliuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulio lililotokea katika soko la ng'ombe la Kompiembiga , kilomita 15 na mji wa Pama, Mashariki mwa nchi Jumamosi Mei 30, wakati raia watano na maafisa wa polisi watano waliuawa huko Foube.