Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

DRC: Kesi mpya za maambukizi ya Ebola zaripotiwa Equateur

Mlipuko huo unaendelea tangu Agosti 2018 katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri, ambapo watu 2,300 wamefariki dunia.
Mlipuko huo unaendelea tangu Agosti 2018 katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri, ambapo watu 2,300 wamefariki dunia. REUTERS/Goran Tomasevic/File Photo
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Mkoa wa Equateur, Kaskazini Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umerekodi kesi mpya za ugonjwa wa virusi vya Ebola, Waziri wa Afya, Eteni Longondo, ametangaza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Kinshasa Jumatatu wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Eteni ametangaza kulingana na matokeo ya sampuli kutoka Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa magonjwa ya kuambukia (INRB), ambazo zimepatikana na virusi vya Ebola.

Ameahidi kwenda katika mji wa Mbandaka katika siku zijazo kusaidia timu za kuzuia na kudhibiti magonjwa ya kuambukia.

Watu wanne wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo hatari, ametangaza Waziri wa Afya Eteni Longondo.

Mwaka wa 2018, mkoa wa Equateur ulikumbwa na mlipuko wa Ebola kwa mara ya 9 hasa katika eneo la Bikoro. Mlipuko huo ulitangawza kumalizika mwezi Julai mwaka 2018. Watu 33 walifariki dunia na 21 walipona.

Mlipuko huo unaendelea tangu Agosti 2018 katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri, ambapo watu 2,300 wamefariki dunia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.