Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SUDAN-UHASAMA-USALAMA

Hali ya utulivu yarejea kwenye mpaka wa Ethiopia na Sudan

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan akitawazwa kama rais wa Baraza Kuu tawala nchini Sudan, Karthoum, Agosti 21, 2019 (picha ya kumbukumbu).
Jenerali Abdel Fattah al-Burhan akitawazwa kama rais wa Baraza Kuu tawala nchini Sudan, Karthoum, Agosti 21, 2019 (picha ya kumbukumbu). SUDAN PRESIDENTIAL PALACE / AFP

Ethiopia na Sudan zinajaribu kuzuia uhasama baina ya raia wa nchi hizo mbili baada ya vurugu kutokea kwenye mpaka wa nchi hizo siku ya Alhamisi wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo wa Amhara, wakisaidiwa na jeshi la Ethiopia, walilipenya na kuingia mara kadhaa katika ardhi ya Sudan. Mapigano yalizuka, na kusababisha kifo cha afisa mmoja wa Sudan na raia kadhaa.

Wakati huo huo serikali ya Khartoum ilimuitisha mwanadiplomasia anayehusika na maswala ya nje kwenye ubalozi wa Ethiopia nchini Sudan na kutangaza kutuma majeshi yake kwenye nchi hiyo na Ethiopia.

Lakini Jumapili Mei 31, pande hizo mbili ziliweka kando tofauti zao na kujaribu kuzuia kutokea kwa machafuko zaidi.

Jumapili Mei 31 serikali ya Khartoum iliamua kupunguza jazba wakati msemaji wa jeshi alipopendekeza kufanyika kwa doria za pamoja kati ya majeshi ya Sudan na Ethiopia kuhakikisha usalama kwenye eneo la mpakani. Katika mchakato huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia imekubali hoja hiyo na kuzungumzia juu ya uwezekano wa kuwepo kwa "mazungumzo ya pamoja", ikitoa rambi rambi zake kwa familia za wahanga. Serikali ya Addis-Abba imependekeza kuwepo kwa uchunguzi wa pamoja.

Wakulima wa Ethiopia kwa miaka mingi, wamekuwa waendesha shughuli za kilimo upande wa Sudan. Inasemekana kwamba walirahisishiwa kwa shughuli zao hizo na utawala wa Sudan wakati huo, kufuatia makubaliano kati ya Omar al-Bashir na kiongozi wa Ethiopia, Méles Zenawi, katika miaka ya 1990. Kwa hatua hiyo, vikosi vya Ethiopia kwa upande wake vililazimika kuzuia waasi wa Sudan kupata hifadhi ya ukimbizi nchini Ethiopia na kutumia nchi hiyo kwa kuendesha mashambulizi dhidi ya Sudan.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.